Vitabu vya maisha ya kiroho


Kanisa la Biblia Publishers

Huduma za Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu anavyosaidia katika uamsho na kutoa vipawa mbalimbali
Detmar Scheunemann
Kurasa 186

Huduma hizo zinachunguzwa katika mazingira ya uamsho wa kiroho uliotokea Indonesia. Kitabu hiki ni mwalimu mzuri sana wa somo la huduma hizo. Wachungaji wengi wanaohangaika usiku na mchana kupata kitu cha kusaidia ili Wakristo wakue kiroho, hivyo wana msaada mkubwa sana. Kitabu kimeandikwa katika mazingira yanayofanana na hali ya kiroho katika Afrika Mashariki tunapoona uamsho na kazi na matendo makubwa ya Roho Mtakatifu katika kanisa lake.

Mwandishi Detmar Scheunemann ni mwalimu wa Biblia anayetoa huduma zake za kujenga kanisa kiroho huko Ujerumani na Indonesia.
Kanisa la Biblia Publishers

Imani Yetu ndiyo Ushindi

Biblia Inasema Nini Kuhusu Mungu, Ulimwengu, Dhambi, Wokovu, Kanisa, Mambo Yajayo, Maandiko Matakatifu
Hans Legiehn
Kurasa 216

Wakristo wengi wanajiuliza, “Imani yangu ni nini?” Maelezo yote katika kitabu hiki yanaonesha Biblia inayosema kuhusu imani hiyo. Watu wanapoelewa mafundisho ya msingi wa imani kufuatana na Biblia wanaimarika na wanaweza kushuhdia vizuri zaidi.

Hapo mafundisho ya msingi kuhusu imani ya Kikristo yanaelezwa katika mafungu saba. Biblia inasema nini kuhusu Mungu, Ulimwengu, Dhambi, Wokovu, Kanisa, Mambo Yajayo na Maandiko Matakatifu? Kitabu hiki kinafaa sana kwa kujifunza na kufundisha Neno la Mungu. Kinatoa mwanga mkali kwa kuonesha mafundisho ya ukweli wa wokovu katika Biblia. Mafundisho ya Biblia juu ya imani na mafundisho ya mambo makuu ya historia ya wokovu yameunganishwa vizuri sana.

Masomo hayo juu za imani ya kikristo hasa ni kwa ndugu wengi wanaotaka kukua na kuimarika katika imani yao. Imani yao iwe ushindi uushindao ulimwengu. Na kwa wote wanaotaka kuwafundisha wengine, kitabu hiki kiwe kiongozi na mwalimu kwa habari ya njia ya Mungu kwa wanadamu, na njia ya wanadamu kwa Mungu jinsi ionekanavyo katika Biblia.
Kanisa la Biblia Publishers

Maombezi

Fay Smart
kurasa 32

Maombezi ni dua au kusihi kwa niaba ya mwingine. Kitabu hiki kinajibu maswali mengi kuhusu huduma ya maombezi.
  • Roho Mtakatifu anasaidiaje maombi yetu?
  • Je, ni mambo gani yanayoweza kufanya maombi yetu yasifae?
  • Je, ni vipi kuhusu ombi ambalo halijajibiwa?
Kanisa la Biblia Publishers

Je, Unajitahidi Kupata Nini, Taji au Wokovu?

Yoshua Ekipikhe
kurasa 28

Mungu anatoa kipawa cha uzima wa milele, lakini vilevile anataka kutoa thawabu kubwa kwa watoto wake wanaomtumikia. Kitabu hiki kitakusaidia kuelewa tofauti iliyopo kati ya kujitahidi kupata wokovu na kupata taji zilizoahidiwa.
Kanisa la Biblia Publishers

Matatizo ya Tamaa Mbaya

William McDonald
kurasa 16

Matatizo ya tamaa mbaya yapo. Usidhani kwamba wewe peke yako unaweza kusimama bila kuanguka. Lakini kuna tumaini: kuna ushindi kwa utukufu wa Bwana Yesu Kristo siku hadi siku.
 

Wasiliana nasi

Kanisa la Biblia Publishers
P.O.Box 1424, Dodoma
Tanzania

Phone: +255 (0) 26 2354 500
Mobile: +255 (0) 713 609166
Email: contact@klb-publishers.org

Location: Dodoma, Ipagala,
Eneo la Emmaus, off Dar Road

Washiriki wetu