Vitabu kwa viongozi


Kanisa la Biblia Publishers

Wito wa Viongozi wa Kikristo

Mifano ya Kanisa, Injili na Huduma kutoka katika 1 Wakorintho 1 – 4
John Stott
Kurasa 102

Waraka wa kwanza kwa Wakorintho sura nne za kwanza zina ujumbe unaohusu sana viongozi wa Kikristo katika ulimwengu wa leo. Kuna ujumbe wa pekee kwa ajili ya viongozi wa kanisa la leo, wawe ni wasimikwa au ni walei, wenye huduma ulimwenguni au kanisani.

Katika sura nne za kwanza za waraka huo, sehemu ya maandiko ambayo ni msingi wa kitabu hiki, Paulo anajibu hoja mbalimbali kutokana na hali ya machafuko mengi ya kuingiliana huko Korintho, na kwa maswali ambayo Wakorintho walikuwa wakimwuliza. Anafanya hivi kwa uwazi, busara, unyenyekevu, upendo na upole wa kuvutia sana: sifa na tabia za kiuchungaji ambazo zinahitajika sana kwa viongozi wa Kikristo hadi leo. Hivyo John Stott anaonesha umuhimu wa “Nguvu Kupitia Udhaifu.”
Kanisa la Biblia Publishers

Uongozi wa Kiroho

Toleo lenye Nyongeza na maswali kwa vikundi.
J. Oswald Sanders
Kurasa 168

Kitabu hiki kinatumiwa hasa kwa kuandaa na kufundisha viongozi. Spiritual Leadership ni kitabu kinachofahamika sana na viongozi wengi walifaidika na kuchongwa na kitabu hiki. Kina mafundisho yenye manufaa kwa maisha na kazi ya watumishi wa makanisa yote. Mifano ya viongozi wa Biblia yanaonyeshwa katika maisha ya Petro, Paulo na Nehemia. Baina ya mawazo makuu yanakuwa: “Mahitaji ya Kiongozi,” “Uwezo wa kugawa madaraka” na “Kiongozi na kuomba kwake.”

Mwandishi J. O. Sanders alitoa mafundisho hayo kati ya miaka 1964-66 kwenye mikutano ya wamisionari Singapore. Baada ya kutoa mafundisho katika kitabu kiliendelea kusomwa na viongozi wengi kwa lugha nyingi. Hapo tunatoa toleo jipya kabisa kufuatana na jinsi kitabu kilivyohaririwa upya na watoaji wa kimarekani Moody Press pamoja na nyongeza ya maneno na sura mbili. Sasa mtiririko wa kujisomea ni rahisi zaidi na ujumbe wake unaeleweka vizuri zaidi. Pia tulitafsiri maswali kwa kujadili katika vikundi ili kitabu kiweze kutumika katika masomo na warsha mbalimbali.
Kanisa la Biblia Publishers

Mtumishi Mwaminifu wa Yesu

Kumfuata Bwana Yesu kama wanafunzi wake walivyomfuata
William MacDonald
Kurasa 83

Kitabu hiki kinajaribu kufundisha masharti ya kuwa mfuasi wa Bwana Yesu kama zilivyotajwa katika Agano Jipya. Baadhi yetu tumeona kanuni hizo katika Neno la Mungu kwa muda mrefu, lakini tunafikiri ni vigumu kuzihusisha katika maisha yetu ya siku hizi za mabadiliko na maendeleo ya kisayansi na teknolojia. Hivyo tunapoa kiroho kwa kuzoea hali na mazingira ya dunia hii.

Jifunze kuhusu vipingamizi vya kumfuata Yesu, maombi, utumishi na ndoa, vita ya kiroho na maswala mengi mengine.
Kanisa la Biblia Publishers

Kanisa la Kitabu

Makanisa yalitokea watu waliposoma kitabu
R.E. Harlow
Kurasa 116

Mtindo huu wa kuanzisha makanisa ni masimulizi kuhusu kundi la vijana walivyoanzisha kanisa kwa kutumia “kitabu” kimoja tu. Waliweza kufuata maagizo ya Agano Jipya tu, na hivyo walijenga kanisa lao dogo sawasawa na mfano wa yale waliyosoma katika kitabu cha Agano Jipya.

Kitabu hiki kimepangwa katika maigizo 12 kufuatana na mwaka mmoja. Kila igizo linafundisha mambo kadhaa yanayoandikwa katika jumlisho fupi mwishoni mwa sura. Hivyo wanaosoma au wanaosikia igizo wanaelewa kwa urahisi mtindo wa kanisa la Agano Jipya. Kitabu hiki kinafaa sana kwa kusomwa katika vikundi vidogo vidogo.
 

Wasiliana nasi

Kanisa la Biblia Publishers
P.O.Box 1424, Dodoma
Tanzania

Phone: +255 (0) 26 2354 500
Mobile: +255 (0) 713 609166
Email: contact@klb-publishers.org

Location: Dodoma, Ipagala,
Eneo la Emmaus, off Dar Road

Washiriki wetu