Historia
Kanisa La Biblia Bookshop in DodomaVitabu vya kwanza „Panorama ya Biblia“ na „Imani yetu Ndiyo Ushindi“ vilitolewa mwaka 1980 na kuchapishwa na Nusch-Druck Gummersbach, Ujerumani. Vitabu vyote viwili vilitafsiriwa kutoka Kijerumani na Helmut Gräf, aliyekuwa mwanzilishi wa Chuo cha Biblia Nanjoka, Tunduru Mkoa wa Ruvuma, Tanzania. Palikuwa na uhitaji wa kuandika au kutafsiri vitabu vinavyoeleza Biblia kwa walimu na wanafunzi wa Biblia Afrika Mashariki.

Kisha Helmut Gräf alianza kutafsiri ufafanuzi wa Agano Jipya katika vitabu 5 vinavyoitwa “Agano Jipya Lasema” No. 1 hadi 5, na badaye aliongeza vitabu 10 vya “Agano la Kale Lasema” No. 1 hadi 10.Huu ni ufafanuzi wa kwanza wa Kiswahili wa Biblia nzima. Mfululizo una vitabu 15 na ulitolewa mwaka 1986 hadi 1990. Badaye vitabu vyote 15 vilijumlishwa katika kitabu kimoja kinene kinachoitwa “Bibla Inasema” na kutolewa mwaka 2000 Dodoma. Kazi ya kusambaza vitabu haikuwa rahisi kutoka Tunduru, kusini mwa Tanzania. Kwa hiyo Kanisa la Biblia Publishers walihamia kwenye mji mkuu wa Tanzania Dodoma. Kutoka hapo katikati ya nchi usambazaji uliendelea vizuri tangu mwaka 1993.

Wakati wa ujenzi wa kituo cha maandiko Dodoma kuanzia mwaka 1991 Nd Helmut Gräf aliendelea kutafisiri “Kamusi ya Biblia” kutoka kiingereza. Kitabu hiki muhimu cha rejea kilichoandikwa na Don Fleming kilitolewa Dodoma mwaka 1995.

Hatua nyingine kubwa ilikuwa kutafsiri na kutoa vitabu viwili vya Erich Sauer kutoka Kijermunai kuhusu historia ya wokovu. Vitabu viwili “The Dawn of World Redemption” na “The Triumph of the Crucified” vilitolewa mwaka 2003 katika kitabu kimoja kinachoitwa “Ufunuo wa Mungu na Itikio la Imani”. Kwa kutumia kitabu hiki msomaji wa “Panorama ya Biblia” anaelewa vizuri zaidi historia ya Mungu na wanadamu. Kitabu cha mwisho kilichotolewa kimeandikwa na John Stott na kinaitwa „Wito wa Viongozi wa Kikristo“. Kitabu hiki kinafundisha mikakati ya uongozi kufuatana na 1 Wakorintho sura ya 1 hadi 4.
 

Wasiliana nasi

Kanisa la Biblia Publishers
P.O.Box 1424, Dodoma
Tanzania

Phone: +255 (0) 26 2354 500
Mobile: +255 (0) 713 609166
Email: contact@klb-publishers.org

Location: Dodoma, Ipagala,
Eneo la Emmaus, off Dar Road

Washiriki wetu