Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Je, mnachapa kitabu changu?
Hapana hatuwezi kuchapa vitabu. Sisi tunachapa baadha ya vitabu vyetu na Inland Press Mwanza. Tunaomba uulizie huko.

2. Je, mtapokea kitabu changu na kukitoa?
Tunasikitika kwamba kwa sasa hivi hatuna uwezo wa kuhariri kitabu chako. Wasiliana na Tanzania Evangelical Literature Ministry, P.O.Box 1009, Morogoro, Tanzania ili wakusaidie kumpata mhariri au mtoaji wa kitabu chako kwa kiswahili.

3. Je, tutapata kipunguzo kwa vitabu vyenu?
Ndiyo, tunatoa vipunguzo kufuatana na orodha yetu ya bei za vitabu. Agiza orodha ya bei hapo chini.

4. Mnatoa vitabu bure?
Tunasikitika kwamba hatuwezi kufadhili huduma na vitabu. Ukiagiza vitabu unavyohitaji unahitaji kumtafuta mfadhili kwa njia yako. Tunaweza kukuambia njia za kulipa ndani ya Tanzania na nje pia.

5. Kwa nini mnatoa kwa Kiswahili tu?
Tunatoa vitabu vilivyotafsiriwa au kuandikwa kwa Kiswahili tu, kwa sababu tunaona umuhimu wa wahudumu kuhubiri na kujiandaa kwa kiswahili. Tunashindwa kujihusisha na lugha zingine.
 

Wasiliana nasi

Kanisa la Biblia Publishers
P.O.Box 1424, Dodoma
Tanzania

Phone: +255 (0) 26 2354 500
Mobile: +255 (0) 713 609166
Email: contact@klb-publishers.org

Location: Dodoma, Ipagala,
Eneo la Emmaus, off Dar Road

Washiriki wetu